19 Machi 2011 - 20:30

Serikali ya Pakistan imeipa Marekani siku 15 kuhamisha kituo chake cha kijeshi cha anga nchini humo baada ya mashambulizi ya ndege za kivita za shirika la kijeshi la nchi za Magharibi NATO kusababisha mauaji karibu na mpaka wa nchi hiyo na Afghanistan.

Mashambulizi hayo yamesababisha kuuawa askari 28 wa Pakistan na kujeruhiwa wengine 15 huko kusini magharibi mwa nchi hiyo. Kituo hicho cha kijeshi cha Shamsi kimekuwa kikitumika kama eneo la siri la kufanyia mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za CIA. Pakistan pia imetoa amri ya kuangaliwa upya makubaliano yote yaliyofikiwa kati yake, Marekani na NATO yakiwemo ya kidiplomasia, kisiasa, kijeshi na shughuli za kijasusi. Uamuzi huo umechukuliwa baada ya Waziri Mkuu wa Pakistan Yousuf Raza Gilani kufanya makutano wa dharura na Baraza la Mawaziri pamoja na maafisa wa jeshi la Pakistan.